Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Saleh Possi awasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais Dr. Frank-Walter Steinmeier jijini Berlin

Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Dr. Abdallah Saleh Possi -- ambaye anamwakilisha Rais pia nchini Uswisi, Austria, Poland, Jamhuri ya Cheki, Slovakia, Romania, Bulgaria na Hungary -- aliwasilisha hati za utambulisho kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa Mh. Rais wa Ujerumani Dr. Frank-Walter Steinmeier jijini Berlin hapo tarehe 06/06/2017.

  • Pichani ni msafara wa Mhe. Balozi mteule Dr. Abdallh Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani akiwasili katika eneo la Ofisi ya Rais wa Ujerumani kwa ajili ya kuwasilisha hati za utambulisho.
  • Pichani ni Mhe. Balozi mteule DR. POSSI akiweka saini katika kitabu Maalumu kabla ya kuwasilisha hati za Utambulisho kwa Rais wa Ujerumani.
  • Balozi Mteule akiwa mbele ya Gwaride lililoandaliwa maalumu kwa heshima ya Balozi Mteule Dr. Abdallah Saleh Possi kabla ya kukabidhi hati za utambulisho.
  • Balozi mteule DR. Abdallah Saleh Possi akipokea heshima kutoka kwa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa heshima yake kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Ujerumani tarehe 06/06/2017. Nyuma ni maafisa Ubalozi, maafisa wa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani pamoja na Familia ya Mh. Balozi DR. Abdallah Saleh Possi.
  • Mh. Balozi Dr. Abdallah Saleh Possi akikabidhi hati kwa Rais wa Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier
  • Balozi Dr. Abdallah Saleh Possi akipeana Mkono na Rais wa Ujerumani Mhe. Frank-Walter Steinmeier mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Joseph Magufuli.
  • Mh. Balozi Dr. Abdallah Saleh Possi (wa tatu kutoka Kulia) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani pamoja na familia yake mara Baada ya kukabidhi hati za utambulisho tarehe 06/06/2017.